1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaongeza mashambulizi Ukraine

16 Aprili 2026

Mashambulizi ya anga ya Urusi yameua takriban watu 14 na kujeruhi wengi Ukraine, yakiharibu majengo na kuongeza wito wa Kyiv kwa msaada zaidi wa kimataifa.

Urusi-Ukraine
Huduma za uokoaji zimefanikiwa kumwokoa mtoto mmoja kutoka kwenye kifusi cha jengo la ghorofa.Picha: Russland-Ukraine-Krieg/picture alliance/AP

Takriban watu 14 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na Urusi katika maeneo mbalimbali ya Ukraine usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa maafisa wa Urusi meya wa Kiev Vitali Klitschko watu wanne wameuwawa na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo akiwemo mtoto wa miaka 12, huku wakazi wakihimizwa kuendelea kujificha katika maeneo salama kutokana na mashambulizi zaidi.

Ripoti zinaeleza kuwa milipuko kadhaa imesikika katika mji huo huku majengo ya makazi na biashara yakiharibiwa katika wilaya mbalimbali. Huduma za uokoaji zimefanikiwa kumwokoa mtoto mmoja kutoka kwenye kifusi cha jengo la ghorofa, ambapo yeye na mama yake wanapatiwa matibabu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa wito mpya kwa washirika wa Ukraine kuendelea kuiunga mkono nchi hiyo na kutekeleza ahadi za misaada kwa wakati, akisema mashambulizi haya yanaonyesha umuhimu wa kuendelea kuiwekea Urusi shinikizo la kimataifa.

"Ni muhimu kuendeleza shinikizo linalohitajika dhidi ya Urusi kuhusu vita hivi — ikiwa ni pamoja na vikwazo, kuzuia kuifanya irudi katika hali ya kawaida kimataifa, na kuhakikisha Ukraine inapokea msaada wa kutosha. Haya yote ni muhimu kwa ajili ya amani. Na leo tumesisitiza hasa umuhimu wa kuondoa vikwazo vinavyokwamisha kifurushi cha msaada wa Umoja wa Ulaya kwa Ukraine chenye thamani ya euro bilioni 90. Uamuzi huu ni wa lazima."

Katika mji wa Dnipro, watu wawili wameuawa na 27 kujeruhiwa kufuatia shambulizi la kombora, huku baadhi ya majeruhi wakiwa katika hali mbaya na majengo kadhaa yakiteketea kwa moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW