Urusi yaonya kuhusu uwanachama wa Finland katika NATO
4 Aprili 2023Urusi imeutaja uanachama wa Finland katika jumuiya ya NATO kuwa ni uvamizi dhidi ya usalama wake na kusema itachukua hatua. Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi habari mjini Moscow kwamba hatua hii ni shambulizi dhidi ya masilahi ya Urusi na wanalazimika kuchukua hatua za kiufundi na kimkakati bila kutoa maelezo zaidi. Finland imejiunga na NATO leo na kuwa mwanachama wa 31 wa muungano huo wa kijeshi.
Soma pia: Finland kujiunga rasmi na NATO siku ya Jumanne
Katika taarifa tofauti wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema kwa kujiunga na NATO, Finland imejipoteza yenyewe na uhuru wowote ilionao.
Wizara hiyo pia imesema hatua zaidi za Urusi zitategemea kanuni za NATO kuijumuisha Finland ikiwa ni pamoja na upelekaji wa miundombinu ya kijeshi na mifumo ya silaza za mashambulizi katika himaya yake.