1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaonyesha kutojali mustakabali wa OSCE

2 Desemba 2023

Shirika la Usalama na Ushirikiano Ulaya OSCE ambalo ndilo shirika kubwa zaidi la usalama wa kikanda duniani, limekamilisha mkutano wake wa kilele wa kila mwaka huku Urusi ikionyesha kutojali mustakabali wa shirika hilo.

Nordmazedonien Außenminister Lawrow zu Besuch
Picha: Russian Foreign Ministry Press/TASS/dpa/picture alliance

Katika hotuba yake, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema, hajali kuhusiana na mwelekeo wa shirika hilo kwa kuwa limekuwa kile alichokiita, kiambatisho cha jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya.

Malta ndiyo nchi iliyochaguliwa kama mwenyekiti mpya na mwandalizi wa mkutano ujao mwakani, ambapo imeichukua nafasi ya Estonia ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ambayo Urusi ilipinga nchi hiyo kupewa uenyekiti.

Lengo la shirika hilo ni mijadala ya masuala ya usalama ingawa Urusi imekuwa ikizuia maamuzi muhimu ya shirika hilo lenye wanachama 57.

Ukraine inaitaka OSCE iufutilie mbali uanachama wa Urusi la sivyo shirika hilo litasambaratika polepole.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW