1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yapinga azimio la kusitisha vita Sudan

19 Novemba 2024

Urusi jana Jumatatu ilitumia kura yake ya turufu kulizuia azimio la Umoja wa Mataifa lililopendekeza usitishaji wa vita mara moja nchi Sudan, kati ya jeshi rasmi na wanamgambo.

UN-Sicherheitsrat 2024 | Abstimmung über Sudan-Resolution scheitert an russischem Veto
Wajumbe wa Baraza la Usalama wakipigia kura rasimu ya azimio linalolenga kuendeleza hatua za kulinda raia nchini Sudan mjini New York, Novemba 18, 2024.Picha: Lev Radin/Sipa USA/picture alliance

Azimio hilo lilipendekeza pia hatua ya kupelekwa msaada wa kibinadamu kwa mamilioni ya watu wanaohitaji. China ambayo ni mshirika wa Urusi pamoja na mataifa mengine wanachama waBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waliliunga mkono azimio hilo lilowasilishwa na Uingereza pamoja na Sierra Leone. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Lammy, aliyeongoza mkutano huo katika Umoja wa Mataifa aliliambia baraza hilo kwamba hatua ya Urusi ni fedheha. Katika wiki za hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulitahadharisha kwamba Sudan imeshafika ukingoni kutumbukia kwenye baa la njaa.