1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yarusha ndege 38 zisizokuwa na rubani Ukraine

18 Novemba 2023

Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi imerusha ndege 38 zisizokuwa na rubani kuelekea nchini humo usiku kucha, hiyo ikiwa idadi kubwa zaidi ya mashambulizi ya droni kuripotiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki sita.

Shambulizi la droni katika anga ya Kyiv
Ndege isiyokuwa na rubani iliyorushwa na UrusiPicha: Gleb Garanich/Reuters

Ukraine lakini imesema imeziharibu droni 29 kati ya 38 za "kamikaze" zilizorushwa na Urusi. Jeshi la Ukraine limeendelea kusema kiwanda kimoja cha nishati kimeshambuliwa kusini mwa Odesa na moto uliozuka kuzimwa kwa haraka. Nayo wizara ya ulinzi ya Urusi imesema pia kwamba imeidungua droni ya Ukraine katika eneo la mpakani la Bryansk. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema anatarajia Urusi izidi kuishambulia miundo mbinu yake ya nishati kwa ajili ya kulemaza usambazaji wa umeme na joto majumbani katika miezi ya majira ya baridi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW