1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema Assad ameondoka nchini Syria

8 Desemba 2024

Mshirika wa karibu wa Assad, Urusi, kupitia wizara yake ya kigeni imesema rais wa Syria Bashar al Assad ameondoka madarakani na kuitoroka nchi huku akitoa maagizo ya ukabidhi wa madaraka kufanyika kwa amani.

Putin na Assad
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa na Rais wa Syria Bashar al AssadPicha: SANA/AFP

Katika taarifa yake, wizara hiyo haikusema alipo Assad lakini imesisitiza kuwa Urusi haikuhusika na mazungumzo ya kuondoka kwake. 

Moscow ilikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya matukio ya Syria na kuhimiza pande zote kujizuwia na vurugu na kusuluhisha masuala yote ya uongozi kupitia njia za kisiasa. Urusi imesema inawasiliana na makundi yote ya upinzani Syria kuhakikisha hilo linafanyika. 

Waasi wa Syria watangaza marufuku ya kutembea nje usiku baada ya kuuangusha utawala wa Assad

Urusi pia imesema kambi zake za kijeshi Syria ziko katika tahadhari kubwa lakini hakuna kitisho dhidi yao kwa sasa. 

Abu Mohammed al-Golani, kamanda wa zamani wa kundi la Qaida aliyekata mafungamano yake na kundi hilo miaka mingi iliyopita anaongoza kundi kubwa la waasi nchini Syria na anatarajiwa kuhusika kutoa muelekeo wa mustakabali wa taifa hilo. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW