Urusi iko tayari kuanza mazungumzo ya amani
8 Desemba 2024Matangazo
Msemaji wa Ikulu hiyo Dmitry Peskov amesema majadiliano ya amani yanatakiwa kujikita kwenye makubaliano yaliyofikiwa Istanbul mwaka 2022 na kwa kuzingatia pia hali ya sasa katika uwanja wa mapambano.
Peskov amesema Ukraine imeacha kuwasiliana na uongozi wa Urusi kupitia amri maalum na iwapo mazungumzo yatatakiwa kuendelea hali hiyo inapaswa kuondolewa.
Trump asema Zelensky ana nia ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine
Kauli ya Peskov imekuja baada ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump kusema rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ana nia ya kuwa na makubaliano ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine baada ya kukutana nae mjini Paris.