1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema imedungua droni mbili za Ukraine mjini Moscow

26 Agosti 2023

Serikali ya Urusi imesema kwamba mifumo ya ulinzi wa anga imedungua ndege mbili za kivita zisiyokuwa na rubani, karibu na mji wa na mjini Shebekino

Russland Sonnenuntergang in Moskau
Picha: Mikhail Metzel/AP Photo/picture alliance

Serikali hiyo imefafanua zaidi na kusema, ndege moja ilidunguliwa ilipokuwa inakaribia mji wa Moscow katika wilaya ya Istrinskii na nyengine katika wilaya ya Shebekino iliyosehemu ya mkoa wa  Belgorod kwenye mpaka na Ukraine. 

Meya wa mji huo Sergei Sobyanin amesema hakuna uharibifu wala majeruhi wowote walioripotiwa kufuatia tukio hilo. 

Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa kutumia droni

Moscow haikuwa inashambuliwa mwanzoni mwa mzozo huo lakini mji huo na miji mingine ya Urusi imelengwa kwa mashambulizi ya Ukraine kupitia ndege zake za kivita zisizokuwa na rubani, huku Kiev ikiapa kuvirejesha vita nchini Urusi baada ya jirani yake huyo kumvamia kijeshi mwezi Februari mwaka jana. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW