1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaharibu boti la Ukraine katika jaribio la shambulizi

2 Septemba 2023

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema mapema leo kwamba vikosi vyake vimeharibu boti la Ukraine ambalo halikuwa na rubani lililotumika katika jaribio la kushambulia daraja linalounganisha rasi ya Crimea na Urusi.

Themenpaket | Getreidehandel Getreide-Deal Grain deal Ukraine Russland
Meli ya TK majestic katika Bahari NyeusiPicha: MEHMET CALISKAN/REUTERS

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, wizara hiyo imesema kuwa hapo jana, jaribio lilifanywa na serikali ya Kyiv la shambulizi la kigaidi kwa kutumia boti iliyopakiwa nusu na isiyokuwa na rubani.

Soma pia:Mashambulizi nchini Urusi yaharibu dhana ya 'jeshi la Putin'

Katika ujumbe kupitia mtandao wa Telegram, wizara hiyo imesema kuwa hapo jana, serikali ya Kyiv ilifanya jaribio la shambulizi la kigaidi kwa kutumia boti iliyopakiwa nusu na isiyokuwa na rubani. Inasemekana kuwa boti hilo liligunduliwa na kuharibiwa kwa wakati katika Pwani ya Bahari Nyeusi.

Ukraine yasema uharibifu wa miundo mbinu ya Urusi ni faida kwake katika vita

Hakukuwa na tamko la haraka kutoka kwa maafisa wa Ukraine ambao kwa kawaida husema machache ama kukaa kimya kuhusu mashambulizi dhidi ya Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW