1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yasema imezima shambulio la Ukraine dhidi ya Crimea

12 Agosti 2023

Urusi imesema leo kuwa imezima shambulio la Ukraine kwa kuzidungua ndege 20 zisizo na rubani zilizoilenga rasi ya Crimia iliyo chini ya udhibiti wa Moscow tangu ilipoinyakua mnamo mwaka 2014.

Daraja la Crimea
Daraja kuu linalounganisha Urusi bara na rasi ya CrimeaPicha: Sergei Malgavko/TASS/picture alliance

Hayo yameelezwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi ambayo imesema ndege 14 ziliharibiwa na mifumo yake ya ulinzi na nyingine sita zilipumbazwa kwa kutumia njia za kielektroniki.

Mashambulizi hayo ya usiku yanafuatia mengine matatu yaliyotokea hivi karibuni yakiulenga mji mkuu wa Urusi, Moscow. Katika hatua nyingine Urusi imedai kurejesha udhibiti wa kijiji kimoja kwenye jimbo la Luhansk baada ya mapambano ya usiku kucha.

Ukraine nayo imeripoti kifo cha kikongwe mmoja kwenye mkoa wa Kharkiv kufuatia shambulizi la kombora la Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW