1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yasema imezuia mashambulizi ya Ukraine ya ndege

1 Agosti 2023

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema leo kwamba imezuia mashambulizi ya Ukraine ya ndege zisizokuwa na rubani kwenye meli zake za kijeshi na kiraia katika Bahari Nyeusi.

Mykhailo Podolyak, afisa katika afisi ya rais wa Ukraine
Mykhailo Podolyak, afisa katika afisi ya rais wa UkrainePicha: Hennadii Minchenko/Avalon/Photoshot/picture alliance

Taarifa ya wizara hiyo imesema meli hizo zilikuwa zinaongoza meli kusini magharibi mwa Sevastopol na zitaendelea na jukumu hilo. Hata hivyo, afisa katika afisi ya rais wa Ukraine, Mykhailo Podolyak, aliyezungumza na shirika la habari la Reuters, imekanusha kwamba imeshambulia meli za kiraia ila afisa huyo amekataa kuzungumzia moja kwa moja madai kwamba jeshi la Ukraine lilishambulia jeshi la majini la Urusi.

Urusi yasema itazishambulia meli zote kutoka bandari za Ukraine

Urusi imesema itazishambulia meli zozote zinazoingia au kutoka katika bandari za Ukraine baada ya mkataba wa usafirishaji nafaka kupitia Bandari Nyeusi kutorefushwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW