1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaunga mkono hatua za Syria dhidi ya waasi

4 Desemba 2024

Urusi imesema inaunga mkono kikamilifu hatua zinazochukuliwa na Syria za kukabiliana na mashambulizi yanayofanywa na wale iliowataja kama "makundi ya kigaidi".

Syrien Opposition Vormarsch Provinz Aleppo
Wafuasi wa upinzani wa Syria wamesimama juu ya kifaru cha jeshi la Syria kilichotekwa katika mji wa Maarat al-Numan, kusini magharibi kutoka Aleppo, Syria, Novemba 30, 2024.Picha: Omar Albam/AP Photo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi Maria Zakharova amesema hii leo kwamba mashambulizi yanayofanywa na waasi katika siku za karibuni yasingewezekana bila ya msaada kutoka nje pamoja na uchochezi.Bila ya kutoa uthibitisho, Zakharova amesema, waasi hao wamesaidiwa ndege zisizotumia rubani na kupewa na mafunzo na mataifa ya kigeni. Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa Rais Bashar al-Assad imekuwa ikiisaidia Syria kijeshi tangu mwaka 2015, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Aidha, Zakharova amesema wanawasiliana kwa karibu na Iran na Uturuki kuhusiana na mzozo huo, kufuatia mashambulizi ya kushtukiza ya waasi, ambao wameudhibiti mji wa pili kwa ukubwa wa Aleppo.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW