1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema Ukraine imeshambulia meli yake Libya

4 Machi 2026

Urusi imeishtumu Ukraine leo kwa kutumia droni za majini kushambulia meli iliyobeba gesi ya asilia katika pwani ya Libya, na kusababisha kuzama kwake.

Meli ya Alexander Obukhov
Uzunduzi rasmi wa meli ya kivita ya Urusi ya Alexander ObukhovPicha: Shamukov Ruslan/ITAR-TASS/picture alliance

Mamlaka ya bandari ya Libya imesema meli hiyo ya mizigo ya Urusi, Arctic Metagaz, ilizama baada ya "milipuko ya ghafla" kaskazini mwa bandari ya Sirte.

Pia imesema meli hiyo ilikumbwa na milipuko ya ghafla iliyofuatiwa na moto mkubwa, ambao hatimaye ulisababisha kuzama kwake kabisa.

Moscow pia imesema meli hiyo ya mafuta ilishambuliwa na droni za Ukraine kutoka pwani ya Libya katika "kitendo cha ugaidi wa kimataifa na uharamia wa baharini".

Pia imesema abiria wote 30 wameokolewa.

Meli hiyo ilikuwa imewekewa vikwazo na Marekani na Umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW