Urusi yashambulia bandari za Ukraine
19 Julai 2023Haya yanafanyika wakati ambapo Urusi imeshambulia bandari za Ukraine, siku moja baada ya kujiondoa kutoka kwenye mkataba wa usafirishaji salama wa nafaka katika Bahari Nyeusi, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Urusi yasema shambulizi lake ni la kulipiza kisasi
Urusi inasema imeshambulia hifadhi za mafuta mjini Odesa na kiwanda kimoja kinachotengeneza ndege zisizokuwa na rubani, kama sehemu yake ya "mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi" kwa shambulizi la Ukraine lililoliharibu daraja la kuelekea Crimea, eneo lililo chini ya utawala wake.
UN yatafakari njia za kusafirisha nafaka za Ukraine na Urusi
Hayo yakiarifiwa, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, amesema kwa sasa wanatafakari njia kadhaa za kusaidia kupeleka katika masoko ya kimataifa, nafaka za Ukraine na Urusi pamoja na mbolea.