1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia gridi ya umeme nchini Ukraine

7 Februari 2026

Urusi imefanya shambulizi kubwa dhidi ya miundo mbinu ya nishati nchini Ukraine na kusababisha kukatika kwa umeme kote nchini humo. Haya yamesemwa leo na Kampuni ya taifa ya umeme nchini humo, Ukrenergo.

Ukraine Jahutyn 2026 | shambulizi la Urusi
Picha inaonyesha matokeo ya mashambulizi ya Urusi katika mji wa Yahutyn katika Mkoa wa Kyiv usiku wa Februari 7, 2026. Picha: Staatlicher Rettungsdienst der Ukraine

Katika ujumbe kwenye mtandao wa telegram, kampuni hiyo imesema mashambulizi hayo bado yanaendelea lakini shughuli ya urekebishaji itaanza mara tu hali ya usalama itakapoimarika.

Waziri Mkuu wa Ukraine Denys Shmygal amesema nchi hiyo imeomba msaada wa dharura kutoka Poland baada ya shambulizi la Urusi dhidi ya vinu vya kuzalisha umeme vya Burshtynska na Dobrotvirska magharibi mwa Ukraine.

Maafisa nchini Ukraine wameishutumu Moscow kwa kulenga miundombinu ya nishati kimakusudi, na kusababisha kukatika kwa umeme ambako kumewaacha mamia ya maelfu ya watu bila umeme wakati wa msimu huu mkali wa baridi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW