1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia gridi ya umeme Ukraine

27 Oktoba 2022

Vikosi vya Urusi vimeshambulia gridi ya umeme katika eneo la katikati mwa Ukraine jana usiku na kusababisha kitisho cha changamoto zaidi ya usambazaji wa nishati.

Ukraine | Zerstörung nach Luftangriffen in Kiew | 17.03.2022
Picha: Vadim Ghirda/AP Photo/picture alliance

Haya yamesemwa mapema Alhamis na mwendeshaji wa gridi hiyo ya Ukrenergo.

Amesema kwenye taarifa kupitia Telegram kwamba kumekuwepo na uharibifu wa vifaa katika mtambo huo mkubwa kabisa wa mifumo ya usambazaji umeme katika maeneo ya katikati mwa Ukraine.

Urusi imeongeza mashambulizi kwenye miundombinu muhimu ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na mitambo ya umeme katika wiki za karibuni, na kuwaacha mamilioni wakikosa umeme na mifumo ya joto kwa muda mrefu wakati majira ya baridi yakikaribia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW