Urusi yashambulia Kharkiv baada ya ziara ya Baerbock
11 Januari 2023Matangazo
Baerbock ameahidi msaada zaidi wa Ujerumani kwa Ukraine, yakiwemo majenerata ya umeme, euro milioni 20 kwa ajili ya kuondosha mabomu ya kutegwa ardhini na milioni 20 kama msaada wa fedha kwa mradi wa Starlink kuhakikisha upatikanaji wa mtandao wa mawasiliano wa intaneti kwa umma.
Waziri Kuleba kwa upande wake amesema hatua ya Ujerumani kukataa kuepeleka vifaru vya mapambano Ukraine inagharimu maisha.
Amesema watu zaidi watakufa kadri inavyochukua muda mrefu kupitisha uamuzi huo na hana shaka Ukraine itapokea vifaru chapa Leopard kutoka Ujerumani.