1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia miundo mbinu ya Ukraine

17 Machi 2026

Mashambulio ya Urusi katika maeneo kadhaa ikiwemo Odessa yameharibu miundo mbinu ya nishati ya Urusi

Zima moto wakidhibiti moto uliosababishwa na mashambulizi ya droni kutoka Urusi dhidi ya miundo mbinu ya usafiri ya Ukraine.
Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Ukraine imesema shambulio la Urusi limesababisha uharibifu wa kiwanda, bandari na miundo mbinu ya nishati katika mkoa wa Odesa usiku wa kuamkia leo.

Ukraine imefahamisha kwamba mashambulizi hayo pia yamesababisha kukatika kwa umeme kwenye baadhi ya maeneo ya makaazi Kusini kwa mkoa huo. Zelenskiy akosoa uamuzi wa kuilegezea Urusi vikwazo

Kwa mujibu wa  Gavana wa Odesa Ole Kiper, kupitia ujumbe alioutowa kwenye mtandao wa Telegram, moto uliosababishwa na mashambulio hayo ulidhibitiwa haraka na kwamba hakuna aliyejeruhiwa.

Urusi pia imeshambulia bandari kubwa ya Ukraine iliyoko kwenye eneo la mto Danube

karibu na Romania ambayo ni mwanachama wa jumuiya ya NATO.

Wizara ya ulinzi ya Romania imesema inachunguza kuhusu tukio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW