1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia miundombinu ya nishati Ukraine

20 Julai 2024

Urusi imefanya mashambulizi kwa kutumia ndege zisizo na rubani katika mikoa mitano ya mashariki, kaskazini na katikati mwa Ukraine. Miundombinu ya nishati ililengwa katika mikoa miwili ya eneo la kaskazini mwa Ukraine

Kiev
Moja ya jengo liloharibiwa na shambulio la Urusi huko Kiev, UkrainePicha: Gleb Garanich/REUTERS

Urusi imefanya mashambulizi kwa kutumia ndege zisizo na rubani katika mikoa mitano ya mashariki, kaskazini na katikati mwa Ukraine. 
Miundombinu ya nishati ililengwa katika mikoa miwili ya eneo la kaskazini mwa Ukraine katika mashambulio hayo ya usiku wa kuamkia Jumamosi.

Soma zaidi. Ursula von der Leyen achaguliwa kuongoza tena Halmashauri ya Ulaya kwa miaka mitano

Kwa mujibu wa jeshi la anga la Ukraine, ulinzi wake wa anga ulifanikiwa kuziangusha ndege 13 zisizo na rubani kati ya 17 zilizotumiwa na Urusi kushambulia mikoa hiyo mitano ya mashariki, kaskazini na katikati mwa Ukraine.

Jeshi limeongeza kusema kuwa hakuna taarifa za watu waliouawa au waliojeruhiwa. Mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani ya Urusi yanayolenga miundombinu ya nishati nchini Ukraine yameongezeka tangu mwezi Machi ambapo yameathiri nusu ya uzalishaji wa nishati hali inayoongeza madhila ya kukosekana umeme kwa mamilioni ya waukraine wanaoishi katika maeneo hayo.