1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yashambulia miundombinu ya nishati Ukraine

25 Novemba 2024

Wanajeshi wa Urusi wameshambulia usiku wa kuamkia leo miundombinu ya nishati kusini mwa Ukraine katika mkoa wa Mykolaiv na viwanda katika eneo la kusini mashariki mwa Zaporizhzhia.

Moja ya miundombinu ya nishati ya Ukraine
Miundombinu ya nishati ya Ukraine hushambuliwa kila wakati na Urusi.Picha: DW

Gavana wa Mykolaiv Vitaliy Kim amesema kupitia mtandao wa mawasiliano wa Telegram kwamba wahandisi wamefanikiwa kurejesha umeme katika sehemu kubwa iliyoshambuliwa.

Gavana huyo amefahamisha kuwa, hakukuwepo majeruhi na kwamba mfumo wa ulinzi wa anga umefanikiwa kuangusha droni mbili zilizoshambulia eneo hilo.

Ama kwa upande mwengine, gavana wa Zaporizhzhia Ivan Fedorov amesema Urusi imefanya mashambulizi kadhaa kwa kutumia droni katika mkoa huo usiku wa kuamkia leo.

Shambulio hilo limesababisha majeruhi ya mtoto mmoja na kuharibu viwanda kadhaa pamoja na jengo moja la makaazi ya watu.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW