1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia miundombinu ya nishati Ukraine

31 Oktoba 2025

Taarifa hiyo ya Zelensky aliyoitowa kwa njia ya video imeongeza kwamba watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kutokana na shambulio hilo na kutoa wito kwa ulimwengu kutofumbia macho kinachoendelea nchini mwake.

Ukraine I 2025
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Urusi imefanya shambulio lingine lililolipua kituo cha nishati nchini humo na kuua watu wawili.

Taarifa hiyo ya Zelensky aliyoitowa kwa njia ya video imeongeza kwamba watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kutokana na shambulio hilo na kutoa wito kwa ulimwengu kutofumbia macho kinachoendelea nchini mwake.

Aidha, kiongozi huyo amevitaja vikwazo vya hivi karibuni vilivyowekwa kwa makampuni ya mafuta ya Urusikama mfano wa majibu kama hayo na kwamba athari zake zinaonekana na vikwazo zaidi kwa Urusi viongezeke ili iweze kusimamisha vita vyake nchini Ukraine.

Hivi karibuni Urusi imeongeza mashambulizi ya anga nchini Ukraine yanayolenga zaidi miundombinu ya nishati.
 
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW