1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia Odesa na kuwauwa watu 2

11 Aprili 2026

Mashambulizi ya droni ya Urusi yamewauwa watu wasiopungua wawili katika mji wa Odesa nchini Ukraine usiku wa kuamkia leo. Haya yamesema leo na mamlaka ya eneo hilo.

Ukraine Odessa 2026 | shambulizi
Uharibifu uliofanywa na shambulizi la droni la Urusi mjini Odesa, Ukraine mnamo Aprili 11, 2026Picha: Oleksandr Gimanov/AFP

Watu wengine wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo wakati droni hizo zilipolenga eneo la makazi, na kuharibu majengo ya ghorofa, nyumba na shule ya chekechea.

Kwa mujibu wa jeshi la wanahewa la Ukraine, Urusi iliilenga Ukraine kwa droni 160 ambapo 133 zilidunguliwa au kunaswa, saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa kwa pendekezo la usitishaji vita kwa sherehe ya Pasaka ya Kiorthodoksi.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia imesema droni 99 zilizorushwa usiku kucha na Ukraine zilidunguliwa kote nchini Urusi na katika eneo la Crimea inayolikalia.

Siku ya Alhamisi, Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kusitisha mapigano kwa masaa 32 mnamo wikendi hii ya Pasaka ya Kiorthodoksi, na kuamuru vikosi vya Urusi  kusitisha mapigano kuanzia saa 4 asubuhi ya leo Jumamosi hadi mwisho wa kesho Jumapili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW