Urusi yataka ihakikishiwe usalama katika mkataba wa Ukraine
26 Desemba 2024Lavrov amesema Moscow inataka mpango wa kisheria utakaoleta amani ya kudumu na kuhakikisha usalama wa Urusi na majirani zake. Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Urusi amesema makubaliano ya kuweka chini silaha kwa muda hayataelekea kokote, akiongeza kuwa Moscow inashuku mpango hafifu wa aina hiyo unaweza kutumika na nchi za Magharibi kuipatia Ukraine silaha zaidi.
Soma pia: Lavrov: Urusi itatumia kila kitu chini ya uwezo wake kuzuia kushindwa vita nchini Ukraine
Aliongeza kuwa Moscow inataka hati za kisheria zitayarishwe kwa njia ambayo inahakikisha kuwa haitowezekana kuyakiuka makubaliano hayo.
Rais wa Urusi Valdmir Putin alisema wiki iliyopita kuwa yuko tayari kulegeza msimamo kuhusu Ukraine katika mazungumzo na Rais mteule wa Marekani Donald Trump kuhusu kumaliza vita hivyo, na hana masharti ya kuanzisha mazungumzo na maafisa wa Ukraine.