Urusi yatishia kuishambulia vikali Ukraine
26 Mei 2026
Serikali ya Urusi imewataka pia raia wa kigeni na wanadiplomasia kuondoka mjini Kyiv haraka iwezekanavyo.
Onyo hilo limekuja baada ya mashambulizi makubwa ya droni na makombora mwishoni mwa wiki yaliyosababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi makumi ya wengine.
Miongoni mwa silaha zilizotumika ni kombora la kasi kubwa la Oreshnik ambalo Moscow inasema lina uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia.
Urusi inadai mashambulizi hayo ni kulipiza kisasi baada ya Ukraine kushambulia shule katika eneo la Lugansk linalodhibitiwa na Urusi. Hata hivyo, nchi za Magharibi zimepuuza vitisho hivyo. Ufaransa na Umoja wa Ulaya zimesema hazina mpango wa kuhamisha wanadiplomasia wao kutoka Kyiv, huku Ukraine ikivitaja vitisho vya Urusi kama mbinu za shinikizo na propaganda za kisiasa.