1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yaushambulia kwa makombora mkoa wa Zaporizhzhia

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Vikosi vya Urusi vimeushambulia mji wa Zaporizhzhia nchini Ukraine kwa makombora leo Jumapili na kuwajeruhi takriban watu 16.

Uharibifu uliotokana na mashambulizi ya Urusi kwenye mkoa wa Ukraine wa Zaporizhzhia
Uharibifu uliotokana na mashambulizi ya Urusi kwenye mkoa wa Ukraine wa Zaporizhzhia.Picha: Ukrainian Emergency Service/AP/picture allaince

Miundombinu kadhaa ikiharibiwa, ikiwemo majengo ya makaazi, biashara pamoja na njia ya reli.

Gavana wa mkoa wa Zaporizhzhia Ivan Fedorov amesema, Urusi imeshambulia wilaya tatu za mkoa huo kwa kutumia jumla ya mabomu 13, na kuongeza kuwa miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika mashambulizi hayo mabaya ni pamoja na watoto wawili.

Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine kupitia mtandao wa Telegram alichapisha picha zilizoonesha athari ya mashambulizi katika mkoa huo wa kimkakati, na kuonesha juhudi za uokoaji manusura zikiendelea. Hata hivyo Moscow haikuzungumzia mara moja shambulio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi