Urusi yaushambulia tena mji wa Kharkiv
23 Septemba 2024Kwa mujibu wa gavana wa mkoa huo, Oleh Syniehubov, majengo 18 yenye ghorofa baina ya 9 na16 yameharibiwa kwa mashambulizi hayo.
Wakaazi kadhaa wa majengo hayo wamelazimika kuhamishiwa maeneo mengine.
Kharkiv ndio mkoa wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara tangu Urusi ilipoanza uvamizi wake mwaka 2022.
Soma zaidi: Zelensky atia saini sheria ya ongezeko la pesa kwa jeshi
Mashambulizi haya yanajiri wakati Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akiwa ziarani nchini Marekani kuomba silaha zaidi za kukabiliana na Urusi.
Akiandika kupitia mtandao wa X, Zelensky amelaani mashambulizi hayo mapya mjini Kharkiv, akiwatolea wito washirika wake wa Magharibi kutuma silaha zaiid kuisaidia Ukraine kuwalinda raia na mali zao.