Urusi yavurumisha takriban droni 400 dhidi ya Ukraine
24 Machi 2026
Matangazo
Mashambulizi makubwa ya droni na makombora kutoka Urusi dhidi ya maeneo ya raia nchini Ukraine, yamewaua watu wanne na kujeruhi wengine 27.
Maafisa nchini Ukraine wamesema hayo siku ya Jumanne mnamo wakati jeshi la Moscow likiongeza juhudi za kuvunja mstari wa mbele wa Ukraine vitani, katika kile kinachoweza kuwa mwanzo wa shambulio la ardhini lililotarajiwa la majira ya machipuko.
Jeshi la angani la Urusi limesema Urusi ilivurumisha takriban droni 400 za masafa marefu dhidi ya Ukraine usiku wa kuamkia Jumanne.
Mashambulizi hayo ambayo ndiyo makubwa zaidi katika wiki ya hivi karibuni, yalirindima hadi mapema siku ya Jumanne ambapo mji mkuu Kiev pia ulilengwa.