1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yawakamata wanaopinga uhamasishaji wa kijeshi

26 Septemba 2022

Jeshi la polisi nchini Urusi limewakamata zaidi ya watu 100 mwishoni mwa juma katika eneo la kusini la Dagestan katika maandamano ya kupinga uhamasishaji wa wanajeshi wa Moscow.

Russland l Proteste gegen Teilmobilmachung l Moskau
Picha: Reuters Photographer/REUTERS

Jeshi la polisi nchini Urusi limewakamata zaidi ya watu 100 mwishoni mwa juma katika eneo la kusini la Dagestan katika maandamano ya kupinga uhamasishaji wa wanajeshi wa Moscow.

Shirika la kufuatilia masuala ya haki za binadamu la OVD-Info, limesema polisi wamewakamata watu wasiopungua 101 huko Makhatchkala, mji mkuu wa Dagestan kusini magharibi mwa Urusi.

Kulingana na hesabu iliyofanywa na vyombo huru vya habari vya Urusi kwa kuziungatia taarifa zilizochapishwa katika mitandao.

Soma zaidi:Kremlin: Ripoti za vijana kuondoka Urusi sio kweli

Dagestan ambayo ni jamhuri maskini yenye Waislamu wengi  imeshuhudia wanaume wengi wakiuawa katika mashambulizi ya vikosi vya Kremlin nchini Ukraine kuliko sehemu nyingine yoyote ya Urusi.

Vyombo vya habari Urusi vilionesha video ya mwanamke akizozana na polisi wakati wa maandamano.

"kwanini mnawachukua watoto wetu" mmoja wa wanawake alisikika katika video akiwauliza kwa ukali polisi wakati wa maandamano hayo ambayo polisi ilitumia nguvu kuyazua.

Katika kile kinachoonekana kutuliza munkari kwa raia, kamishna wa kijeshi wa Dagestan Daitbeg Mustafayev, ambaye anahusika na uandikishaji wa wanajeshi, amesema ni wanaume "wenye ujuzi maalum wa kijeshi" ndio watakaoitwa mara ya kwanza na hakuna watu watakaotumwa Ukrain.

Wengine 13 wauwawa katika shambulio Urusi

Wakati Urusi ikikabiliana na ukosoaji mkubwa wa kile inachokiita uhamasishaji wa kijeshi, watu wengine 13 wameuwawa leo Jumatatu katika shambulio kwenye moja ya shule katikati mwa jiji la Urusi la Izhevsk.

Idara ya huduma ya kwanza na polisi wakiwa katika eneo la tukioPicha: Sergey Kuznecov/SNA/IMAGO

Shambulio hilo la hivi karibunini mfululizo wa matukio ya ufyatuaji risasi shuleni yanayoiandama Urusi kwa miaka ya hivi karibuni wakati ikihamasisha makumi kwa maelfu ya wanaume kujiunga kwa ajili ya kupigana vita Ukraine.

"Watu 13 wameuwawa katika shambulio,wakiwemo walinzi wawili wa shule na walimu wawili" 

Ilisema taarifa iliotolewa na idara ya uchunguzi ya Urusi katika mtandao wa Telegram na kuongeza kuwa watoto 7 ni miongoni mwa waliofariki.

Soma zaidi:Warusi wakimbia baada ya tangazo la uhamasishaji wa kijeshi

 Kwa mujibu wa wachunguzi mshambuliaji huyo ambae ni mwanaume alikuwa kavalia mavazi meusi yakiwa na nembo ya Nazi na hakuwa amebeba kitambulisho chochote na alijiua baada ya kutekeleza shambulio hilo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Urusi imesema kwamba katika tukio hilo watu 20 walijeruhiwa.

Gavana wa mkoa huo Alexander Brechalov amesema miongoni mwa majeruhi hao ni watoto.
    
Ukraine yaendeleza mapambano dhidi ya Urusi
Jeshi Ukraine limesema mlipuko mkubwa umetokea kwenye bandari ya Odesa  kufuatia shambulio la usiku kucha la ndege zisizokuwa na rubani.

Askari jeshi akizungumza na DWPicha: DW

Shambulio hilo limefanyika saa chache baada ya Marekani kuapa kuchukua hatua madhubuti kwa Urusi, endapo zitatumia silaha za nyuklia nchini Ukraine.

Shambulio hilo la anga ni la karibuni zaidi kufuatia mkururo wa mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani kwenye mji huo muhimu wa eneo la Kusini.

Soma zaidi:Scholz autaja uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kuwa ubeberu

Wasiwasi unaongezeka kwamba Urusi inaweza kutaka kuzidisha mzozo huo
mara itakapokamilisha kura ya maoni katika maeneo ambayo inayadhibiti.

Hatua hiyo inayotazamwa na Ukraine na nchi za Magharibi  kuwa ni kinyume cha sheria.

IAEA:Yataka mazungumzo ya amani kati ya Ukrusi na Ukraine
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu nishati ya atomiki alisema Jumatatu yuko tayari kuendelea na mazungumzo nchini Ukraine na Urusi wiki hii ili kuweka eneo la usalama karibu na kinu cha nyuklia.

Wajumbe wa IAEA wakati wa ziara kwenye kinu cha nyukliaPicha: D. Candano Laris/IAEA/dpa/picture alliance

Mapigano karibu na mtambo huo ambao  ni mkubwa zaidi barani Ulaya wa Zaporizhzhia nchini Ukraine  yameibua hofu ya kutokea maafa ya nyuklia.

Soma zaidi:Biden amkosoa Putin, ataka mageuzi Umoja wa Mataifa

Mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA Rafael Grossi, amekutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Ukraine na Urusi kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita kujadili kuweka usalama katika eneo linalozunguka mtambo huo ili kuulinda.

"Hili linawezekana na lazima lifanyike na nipo tayari kuendelea na mashauriano kwa nchi zote mbili" Alisema Grossi katika ufunguzi wake wa mkutano wa mkuu.

IAEA na mataifa  ya Magharibi yalitonesha wasiwasi wao siku ya Jumatano kuhusu usalama wa kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia huku Kyiv ikiishutumu Urusi kwa mashambulizi mapya ya makombora katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW