1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yawatimuwa mabalozi wa Ulaya kuhusu Navalny

5 Februari 2021

Urusi imesema inawafukuza wanadiplomasia wa Sweden, Poland na Ujerumani kwa kushiriki maandamano juu ya Navalny, wakati mkuu wa diplomasia wa EU akizuru taifa hilo.

Russland Präsident Putin
Picha: Mikhail Klimentyev/Kremlin/Sputnik/REUTERS

Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi imesema Ijumaa kuwa mewafukuza wanadiplomasia kutoka Sweden, Poland na Ujerumani kwa kuhudhuria maandamano ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Alexei Navalny.

Wanadiplomasia hao walitangazwa kuwa "watru wasiotakiwa" baada ya kudaiwa kushiriki katika maandamano "haramu" ya kumuunga mkono Navalny Januari 23, imesema wizara hiyo. Maandamano makubwa ya kumuunga mkono Navalny yalifanyika siku hiyo kote nchini Urusi.

Wanadiplomasia kutoka Sweden na Poland mjini St. Petersburg na kutoka Ujerumani mjini Moscow walishiriki maandamano, ilisema, na kwamba matendo yao yalikuwa "hayakubaliki na yasiyofaa kwa hadhi yao ya kidiplomasia.  Walitakiwa kuondoa Urusi "haraka iwezekanavyo", ilisema taarifa ya wizara.

Soma pia:

Tangazo la kufukuzwa kwa wanadiplomasia hao lilikuja baada ya mwanadiplomasia wa juu wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel, kumuambia waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov kwamba namna alivyotendewa Navalny imesababisha ugumu zaidi katika uhusiano kati ya Moscow na Brussels.

Ziara ya Borrel yagubikwa na kisa cha Navalny

Josep Borrel alizuru akikaribishwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov mjini Moscow kwa mazungumzo Februari 5, 2021.Picha: Russian Ministry of Foreign Affairs/TASS/dpa/picture alliance

Josep Borrel alizuru Moscow kwa mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov, wakati ambapo shinikizo la kisheria likiongezeka kuhusu Navalny, na serikali ya nchi hiyo ikikosoa kile ilichokiita maneno ya kibabe kutoka kwa rais wa Marekani Joe Biden.

Mwakilishi huyo wa juu wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya kigeni na usalama aliwasili mjini Moscow siku ya Alhamisi, katika ziara ya kwanza ya mwanadiplomasia wa juu wa umoja huo tangu 2017, wakati mtangulizi wa Borrel, Federica Mogherini alipoizuru Urusi.

"Bila shaka uhusiano wetu umekuwa mgumu sana. Na kesi ya Navalny ndiyo imeongeza ugumu zaidi katika uhusiano wetu. Lakini hatujaunganishwa tu na jigrafia, bali pia masuala kadhaa za uhusiano ya kihistoria, kitamaduni na kiuchumi," alisema Borrel mjini Moscow.

Navalny mwenye umri wa miaka 44 na mchunguzi wa rushwa na mkosoaji maarufu zaidi wa rais Vladmir Putin, alikamatwa mwezi uliopita wakati akirejea kutoka Ujerumani, ambako alikaa kwa miezi mitano akitibiwa kutokana na kupewa sumu, kitendo ambacho anailaumu ofisi ya rais Putin, Kremlin, kukipanga. 

Maafisa wa Urusu wamekanusha tuhuma hizo, huku waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov, akiwatshutumu maafisa wa Ulaya kwa kushindwa kutoa ushahidi kuhusu tuhuma za sumu, na kusema hali ya mvutano haimnufaishi yeyote.

"Lakini tatizo kuu bila shaka ambalo sote tunakabiliwa nalo, ni kushindwa kusawazishaa mambo kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya, kati ya wadau wawili wakubwa zaidi katika anga ya Eurasia. Hii ni hali mbaya ambayo haimnufaishi yeyote."

Alexei Navalny, mpinzani na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Putin.Picha: Babuskinsky District Court/AP/picture alliance/Tass/dpa/picture alliance

Ikulu ya Kremlim imesema haitozingatia ukosoaji wa mataifa ya Magharibikuhusu hukumu ya Navalny na vitendo cha polisi dhidi ya wafuasi wake.

Raia wanazidi kuonyesha kuchoshwa na Putin

Kukamatwa kwake Janauri 17 kulisababisha maandamano makubwa nchini Urusi, wengi wa waandamanaji wakiimba nyimbo za kumpinga rais Putin, katika tukio kubwa zaidi lililodhihirisha kutoridhika katika miaka kadhaa. Maelfu ya waandamani wamekamatwa.

Mahakama ya mjini Moscow ilimtia hatiani Navalny siku ya Jumanne kwa kukiuka masharti ya kifungo chake cha nje katika kesi ya utakatishaji fedha ya mwaka 2014, na ikaamuru atumikie kifungo cha miaka miwili na miezi minane gerezani.

Navalny pia alifikishwa katika mahakama nyingine Ijumaa, akishtakiwa kwa kumtusi veterani wa vita kuu ya pili ya dunia alieonekana kwenye vidio moja ya propaganya ya Kremlin.

Chanzo: Mashirika

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW