Urusi yazidisha mashambulizi dhidi ya waasi wa Syria
1 Desemba 2024Matangazo
Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria limesema mashambulizi ya Urusi ya mapema leo yalilenga miji na vijiji vilivyotekwa na muungano wa upinzani unaoongozwa na wenye itikadi kali huko kaskazini-magharibi mkoa wa Idlib na mkoa wa kati wa Hama. Mashambulio kama hayo pia yaliripotiwa katika mji wa kaskazini wa Aleppo, huko mapema juma hili wanamgambo walifanya mashambulizi ya kushtukiza na dhidi na vikosi vya serikali ya Assad na kuvizidi nguvu. Kwa msaada wa washirika wake Urusi na Iran, al-Assad ameweza kurejesha udhibiti wa takriban theluthi mbili ya nchi kutoka kwa waasi nchini humo katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita.