1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yazidisha mashambulizi nchini Ukraine

28 Desemba 2022

Jeshi la Ukraine limefahamisha kuwa vikosi vya Urusi vilirusha makombora 33 na kuyalenga maeneo ya kiraia yenye watu wengi kwenye ukingo wa kulia wa mto Dnipro karibu na mji wa Kherson.

Ukraine-Krieg - Cherson
Picha: Dimitar Dilkoff/AFP

Wakati mapigano yakipamba moto, Urusi imekanusha kuwalenga raia lakini imetuma katika uwanja wa mapambano vifaru zaidi na magari ya kivita.

Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wiki hii itakuwa muhimu kwa Ukraine kisiasa.

Vikosi vya Urusi viliutelekeza mkoa wa Kherson mwezi uliopita, katika moja ya mafanikio muhimu zaidi ya Ukraine katika vita vilivyodumu kwa miezi 10 sasa.

Moscow imezidisha mashambulizi katika mkoa huo wa Kherson katika dhamira ya kuudhibiti kwa mara nyingine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW