1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yazidisha mashambulizi ya angani Ukraine Mashariki

8 Desemba 2022

Majeshi ya Urusi yanazidisha mashambulizi ya angani na ardhini katika maeneo kadhaa ya makaazi mashariki mwa Ukraine, na haya ni kulinganja na maafisa wa Ukraine.

Ukraine-Krieg | Ukrainische Soldaten mit einem Panzer in Bachmut
Picha: Metin Aktas/AA/picture alliance

Mashambulizi haya ya Urusi yanafanyika siku moja baada ya Rais Vladimir Putin wa Urusi kusherehekea utekaji wa maeneo mengine katika vita hivyo vilivyodumu kwa miezi tisa sasa.

Shirika la habari la Reuters limeripoti mashambulizi katika eneo la makaazi la Bakhmut na maeneo mengine ya Donetsk ambapo raia 9 wameuwawa.

Karibu na mji wa Lysyschansk, Urusi imetuma vikosi zaidi vya wanajeshi kujaribu kukiteka kijiji cha Bilohorivka na kamanda mmoja katika eneo moja la makaazi linalozozaniwa sana, amesema Urusi inazdii kufanya mashambulizi ya angani.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW