1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yazima shambulio la droni za Ukraine mjini Moscow

20 Agosti 2023

Urusi imesema imefanikiwa kuzima shambulio la ndege za Ukraine zisizoruka na rubani dhidi ya Moscow na maeneo yake mengine. Hili ni jaribio la pili la Ukraine kulenga maeneo ya Urusi kujibu mashambulizi ya jirani yake.

Moskau Drohnenangriff auf Hochhaus
Picha: EVGENIA NOVOZHENINA/REUTERS

Kulingana na taarifa ya wizara ya Ulinzi ya Urusi, hii leo alfajiri serikali ya Kiev ilijaribu kutekeleza kile ilichokiita shambulio la kigaidi kwa kutumia droni, dhidi ya miundo mbinu yake mjini Moscow lakini haikufanikiwa. Hakuna majeruhi wala uharibifu wowote ulioripotiwa katika tukio hilo.

Shambulizi la Urusi lawaua watu 7 na kujeruhi 100 Ukraine

Katika kisa kingine droni ya Ukraine ililenga kituo cha treni katika mji wa Kursk ulioko Magharibi mwa Urusi na kuwajeruhi watu watano.

Ukraine imekuwa ikiishambulia Moscow kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani baada ya Urusi kuushambulia mji wake wa Chernihiv na kusababisha mauaji ya watu saba na wengine 150 kujeruhiwa.