1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yadungua droni 31 za Ukraine

20 Januari 2025

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imechapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Telegram kwamba imezidungua droni 31 zilizorushwa na vikosi vya Ukraine ambazo zililenga maeneo yake ya viwanda.

Vita vya Urusi na Ukraine
Mwanajeshi wa jeshi la angala Ukraine akiwa amebeba droni katika eneo la Bakhmut, nchini UkrainePicha: Diego Herrera Carcedo/Anadolu/picture alliance

Wizara hiyo ya Ulinzi imeongeza kuwa mashambulizi hayo ya droni hayakusababisha madhara yeyote lakini haikufafanua zaidi.

Mashambulio baina ya vikosi vya Urusi na Ukraine yameongezeka katika siku za hivi karibuni katika mzozo wao wa karibu miaka mitatu kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump leo Jumatatu.

Trump alisema kwamba anataka kuvimaliza vita hivyo hivi karibuni.

Hapo jana, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameyataka mataifa rafiki wa Ukraine waipe nchi hiyo misaada zaidi ya mifumo ya ulinzi wa anga aina ya Patriot ili nchi yake iendelee kupambana na mashambulizi ya Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW