1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yazitahadharisha meli zinazopitia Bahari Nyeusi

20 Julai 2023

Urusi imesema hapo jana kuwa itazingatia meli zote za mizigo zinazokwenda nchini Ukraine kupitia Bahari Nyeusi kuwa kitisho kwa usalama wake na inaweza kuizishambulia.

Türkei I Istanbul - Schwarzmeer-Getreide-Initiative der Vereinten Nationen
Picha: Mehmet Emin Caliskan/REUTERS

Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imesema vyombo hivyo vinavyoelekea kwenye bandari za Ukraine vitazingatiwa na Moscow kuwa vimebeba shehena ya silaha na mataifa yanayozimiliki yatakuwa yamejiingiza kwenye vita vya Ukraine na yapo upande wa serikali ya Kyiv.

Tamko hilo la Urusi linafuatia uamuzi wake wa siku ya Jumatatu wa kujitoa kutoka mkataba wa kusafirisha nafaka za Ukraine kupitia bandari za Bahari Nyeusi.

Ukraine kwa upande wake imezirai nchini nyingine kwenye kanda ya Bahari Nyeusi kuingilia kati na kuhakikisha usalama wa meli zote zinazotumia ujia huo wa maji.

Serikali ya rais Volodymyr Zelensky imeituhumu Urusi kuwa inalenga kuhujumu kwa makusudi miundombinu ya usafirishaji wa nafaka na mazao mengine ya chakula na kuyaweka hatari mataifa yenye uhitaji duniani

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW