Urusi,Ukraine waafikiana kuwaondoa wanajeshi Azovstal
17 Mei 2022Wanajeshi hao ambao miongoni mwao wamejeruhiwa vibaya walipelekwa katika maeneo ambayo yapo chini ya udhibiti wa vikosi vya Urusi.Ukraine imekataa kuthibitisha kwamba wanajeshi wake wamejisalimisha.
Wizara ya Ulinzi Ukraine ilisema makubaliano hayo ya kuwahamisha wapiganaji wa Ukrainewaliokwama kwenye kiwanda cha chuma, yalifanywa na mwakilishi wa vikosi vya Ukraine ambao bado wamekwama kwenye eneo la kiwanda cha chuma cha Azovstal ambacho kilishubhudia mashambukllizi makali ya vikosi vya Urusi.
Katika zoezi hilo la kuwahamisha wanajeshi hao zaidi ya wapiganaji 260 wa Ukraine ambao waliokuwa wamekwama kwenye eneo hilo mjini Mariupol kwa wiki kadhaa za mashambulizi walifanikiwa kuondolewa.
Kati ya hao askari 53 walijeruhiwa vibaya ambao walipelekwa Novoazovsk, huku 211na waliosalia wameripotiwa kupelekwa Olenivka.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema, uhamishaji wa wanajeshi hao wa Ukraine kutoka katika eneo ambalo linadhibitiwa na vikosi vya Urusi, lilifanyika ili kuokoa maisha ya wapiganaji ambao walivumilia wiki kadhaa za mashambulizi ya wanajeshi wa Urusi wakiwa katika ghorofa ya chini katika kiwanda hicho cha Avostal.
Soma zaidi:Ukraine kusikiliza kesi ya kwanza ya uhalifu wa kivita
Aliongeza waliojeruhiwa wanapata matibabu huku akiahidi kuokolewa kwa wapiganaji wengine zaidi ambao wamekwama kwenye kiwanda hicho.
" Tunatumai kuokoa maisha ya vijana wetu.Miongoni mwao wamejeruhiwa vibaya wamepata matibabu" Alisema Zelensky katika video iliorekodiwa ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida kuelezea mambo yanavyokwendakatika mapigano yanayoshuhudiwa kwa wiki kadhaa sasa.
Alisisitiza kwamba kanuni ya Ukraine ni kuhitaji mashujaa wake wakiwa hai "Nadhani kwa ujumbe huu naweza kueleweka na watu wote vya kutosha."
Wataalamu wahofia wanajeshi zaidi kusalia Azovstal
Uokoaji huo ambao ulfanikishwa na shirika la msalaba mwekundu pamoja na Umoja wa Mataifa wanaendelea na zoezi la kuwaokoa wapiganaji wengine waliosaluiakatika kiwanda hicho cha chuma ambapo inakadiriwa kuwa idadi ya wapiganaji waliokwama katika ineo hilo huenda ikafikia 1000.
Hapo kabla wizara ya ulinzi Urusi ilitanga jana Jumatatu kuwepo kwa makubaliano ya kuwaondoa wapiganaji ambao wamejeruhiwa vibaya waliokwama eneo hilo kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kupelekwa katika eneo ambalo linadhibitiwa na washirika wa Moscow.
Soma zaidi:Vikosi vya Ukraine vyauzuwia msafara wa Urusi kuvuka mto
Katika hatua nyingine Jeshi la Ukraine limesema kupitia mtandao wa Facebook kwamba vikosi vya Urusi kuendelea kulidhibiti eneo la kiwanda cha chuma, kumechelewesha uhamishaji wa wanajeshi 20,000 wa Urusikatika maeneo mengine ya Ukraine hivyo kumezuia Moscow kuteka kwa haraka mji wa kusini wa Zaporizhzhia.
Licha ya misaada mikubwa ya kijeshi inayoipata Ukraine kutoka kwa mataifa jirani, vikosi vyake vimeweza kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Urusi kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa na wengi.