1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urussi na Umoja wa Ulaya kushirikiana zaidi

10 Mei 2005

Mosko:

Urussi na Umoja wa Ulaya leo zimefikia mapatano ya mwisho ya kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja nne muhimu. Mapatano hayo yamefikiwa mjini Mosko katika mazungumzo kati ya Raais Vladmir Putin wa Urussi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya, José Manuel Barroso na Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Waziri Mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker. Nyanja hizo za ushirikiano ni ulinzi wa nje na ndani, uchumi, sayansi na utamaduni. Wanachama wapya wa Umoja wa Ulaya kutoka nchini za Baltic wanataka Urussi ilaumiwe kwa kutumia nguvu. Kinyume chake, Urussi nayo inadai kuwa Warussi, ambao ni wachache, wanakandamizwa Latvia na Esthonia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW