1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

Mawaziri wa biashara Marekani na China wakutana Beijing

Hawa Bihoga
28 Agosti 2023

Waziri wa masuala ya biashara wa Marekani Gina Raimondo amekutana na mwenzake wa china mjini Beijing leo na kusema ni "muhimu mno" kwa mataifa hayo mawili yenye nguvu ya kiuchumi duniani kuwa na uhusiano thabibiti.

China | Gina Raimondo in Peking
Picha: Andy Wong/REUTERS

Ziara hii ni ya karibuni zaidi kati ya mkururo wa ziara za maafisa wa ngazi za juu nchini Marekani kwenye miezi ya hivi karibuni huku Washington ikifanya kila linalowezekana kutuliza mvutano wa kibiashara na Beijing.

Ziara hizo zitafuatiwa na mkutano wa kilele baina ya viongozi wakuu wa mataifa hayo, ambapo Rais wa Marekani Joe Biden alisema hivi karibuni kwamba anatarajia kufanya mazungumzo na mwenzake wa China Xi Jinping mwaka huu.

Soma pia:Marekani yasaka kuimarisha mazungumzo ya kibiashara kati yake na China

Akimkaribisha Raimondo mjini Beijing, waziri wa biashara wa China Wang Wentao amesema anataraji wawili hao kushiriki mazungumzo ya manufaa kwa pande mbili.

"Nafurahi kufanya mazungumzo na uratibu Pamoja nawe." Alisema Wetao baada ya kumkaribisha mgeni wake.

Aliongeza kwamba "mazungumzo haya yatajikita katika nyanja ya uchumi na biashara."

Uhusiano wa Marekani na China ni muhimu duniani?

Raimondo aliikutana leo asubuhi na mwenzake wa china Wang Wentao, akiuelezea uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa yao kama "muhimu zaidi duniani."

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na mwenzake wa China Xi JinpingPicha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na wizara ya biashara ya Marekani, Raimondo amesema biashara kati ya mataifa hayo inafikia kiwango cha dola za Merekani bilioni 700.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba Marekani inautazama uchumi imara wa China kama jambo chanya, kuna haja ya kusawazisha uwanja wa ushindani na kwamba Marekani itafanya kinachohitajika ili kuwalinda wafanyakazi wao.

Soma pia:China kuchukua hatua kuhusiana ziara ya makamu wa rais Taiwan Marekani

Waziri Raimondo alisema timu za pande zote mbili zilifanyakazi katika majira ya joto ili kuanzisha ubadilishanaji wa taarifa na vikundi kazi vitakavyotuwezesha kuwa na uhusiano bora zaidi wa manufaa kwa mataifa yetu mawili.

"Hatua hii itatimiza yale ambayo dunia inayataraji chini ya uongozi wa rais Biden."

Waziri Raimondo atasafiri pia kwenda mji wa kiuchumi wa China wa Shanghai, Washington imesema.

Ziara hizi zitafufua diplomasia ya uchumi?

Uhusiano kati ya Marekani na China umeshuka na kufikia kiwango kibaya kabisa katika miongo kadhaa, ambapo vikwazo vya kibiashara vya Marekani vikiwa juu ya orodha ya mabishano kati ya mataifa hayo mawili.

Washingtona inasema udhibiti huo ni muhimu ili kulinda usalama wake wa taifa, huku Beijing ikiutazama kama njia ya kuzuwia ukuaji wake wa kiuchumi.

Mwezi huu Rais Biden alitoa amri ya rais yenye lengo la kuzuwia baadhi ya uwekezaji wa Marekani katika maeneo nyeti nchini China, hatua ambayo Beijing illikosoa kama inayokwenda kinyume na utandawazi.

Biden na Xi washinikiza ushirikiano katika mkutano wao Bali

02:01

This browser does not support the video element.

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yelen alijaribu kuwahakikishia maafisa wa China kuhusu vizuizi vya Marekani wakati wa ziara mjini Beijing mwezi uliopita, akiahidi kwamba hatua zozote mpya zitatekelezwa katika njia ya uawazi.

Soma pia:Yellen hafikirii kuwa uchumi wa Marekani utashuka

Mnamo mwezi Juni, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken. alifany aziara Beijing ambako alikutana na rais Xi Jinping, na kusema hatua zimepigwa kuhusu masuala kadhaa yanayozusha mabishano.

Mjumbe wa tabianchi wa  Marekani John Kerry pia alizuru China mwezi Julai.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW