1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaionya Serbia kuhusu jeshi lake

30 Septemba 2023

Marekani imeitaka serikali ya Belgrade kuwaondoa wanajeshi wake katika eneo la mpaka wake na Kosovo.

Kosovo Polizei in Mitrovica
Picha: AFP

Marekani imeitaka serikali ya Belgrade kuwaondoa wanajeshi wake katika eneo la mpaka wake na Kosovo, baada ya kubainika kile kilichoelezwa "mkusanyiko mkubwa" wa kijeshi wa Serbia.Msemaji wa Baraza la Usalama wa taifa kwenye kulu ya Marekani, John Kirby aliwaambia waandishi wa habari kwamba wanafuatilia idadi kubwa ya wanajeshi wa Serbia kwenye mpaka na Kosovo.Ikulu ya Marekani imetoa onyo hilo, ikiwa ni baada ya Serbia kupeleka vifaru vyenye uwezo mkubwa na mizinga kwenye eneo hilo la mpaka baada ya mapigano makali kuzuka katika nyumba ya watawa kaskazini mwa Kosovo wiki iliyopita.Katika ghasia hizo afisa wa polisi wa Kosovo na washambuliaji watatu wa Serbia waliuawa, tukio limechukuliwa kama moja ya kisa kibaya kabisa kutokea kwa miaka kadhaa katika eneo hilo la jimbo la Kosovo lililojitenga na Serbia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW