Kikosi cha NATO nchini Ujerumani chakabiliwa na kitisho
23 Agosti 2024Matangazo
Taarifa za kijasusi zimebainisha uwepo wa kitisho. Wafanyakazi ambao sio wa lazima wamerudishwa nyumbani kama hatua ya tahadhari.
Kikosi cha NATO cha ndege za upelelezi, aina ya AWACS, kimewekwa kwenye kituo hicho cha Geilenkirchen, kilichopo karibu na mpaka kati ya Ujerumani na Uholanzi.
Kwa mujibu wa taarifa, NATO imepandisha kiwango cha tahadhari, lakini bila ya kufafanua juu ya kitisho kilichopo.
Wiki iliyopita kituo kikuu cha jeshi la anga la Ujerumani karibu na mji wa Cologne kilifungwa kwa saa kadhaa kutokana na hofu juu ya kuhujumiwa kituo cha ugavi wa maji.