1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushahidi wa Michael Cohen fedheha kwa Donald Turmp

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
28 Februari 2019

Siku moja baada ya kumshutumu Rais Donald Trump kuwa ni mwongo na mbaguzi, mwanasheria wake wa zamani Michael Cohen leo ataendelea kutoa ushahidi wake mbele ya kamati ya upelelezi lakini nyuma ya pazia. 

USA Washington - Michael Cohen vor Aussage
Picha: Getty Images/C. Somodevilla

Ushahidi wa Cohen wa hapo jana Jumatano aliuoutoa bungeni ulikuwa ni fedheha kubwa kwa rais Donald Trump. Kwenye ushahidi huo Bwana Cohen pia alimtaja Trump kuwa ni mtu muongo na mbaguzi. Mwanasheria huyo aliyekuwa wakati mmoja msimamizi wa mipango ya Trump alielezea matukio ambayo Trump aliongopa, ikiwa ni pamoja na malipo ya pesa kwa vimada.

Cohen alisema Trump alisema uongo katika kampeni ya uchaguzi wa 2016 kuhusu maslahi yake ya biashara nchini Urusi na alijua juu ya njama za kumhujumu aliyekuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton. Cohen pia alisema Trump alitoa matamshi yaliyowakejeli watu weusi.

Wajumbe wa chama cha Republican waliokuwa wanamtilia mashaka Cohen walisema mwanasheria huyo alishawahi kukiri kwamba alidanganya bungeni. Rais Donald Trump ambaye alikuwa mjini Hanoi kwenye mkutano kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kusikia ushahidi bandia kama huu wakati akiwa katikati ya mkutano muhimu sana ni jambo la kusikitisha. 

Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Reuters/J. Silva

Trump amesema wakili wake huyo wa zamani ametumia uongo wa hali ya juu na hali kama hiyo haipaswi kutokea kwa rais mwingine yoyote wa Marekani katuka siku za usoni kwa sababu uongo aina hii unaharibu sifa nzuri ya Marekani.

Mara kadhaa Cohen alikataa kutoa maelezo juu ya uhusiano wake na rais wa Marekani, ikiwa ni pamoja na mazungumzo yake ya mwisho na Trump au mwakilishi yoyote wa rais huyo. Kwa mujibu wa Cohen, ni kwa sababu suala hili bado lipo mahakamani mjini New York na kwamba haruhusiwi kulijadili.

Cohen pia aliongeza kusema kwamba anajua kuhusu vitendo vingine visivyo halali vyaTrump, ambavyo bado vinachunguzwa. Alimalizia ushahidi wake kwa kutoa onyo kwamba Trump hawezi kukubali "mabadiliko ya amani ya uongozi" ikiwa hatachaguliwa tena mwaka wa 2020, akisema kuwa Rais huyo atafanya lolote kushinda uchaguzi huo.

Vyanzo: /APE/p.dw.com/p/3EE1V

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW