1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushindi mkubwa Rais Kagame wathibitishwa

24 Julai 2024

Ushindi mkubwa wa Rais wa Rwanda Paul Kagame umethibitishwa katika matokeo ya mwisho, ingawa kumeshuhudiwa kupungua kwa kiwango cha uwakilishi bungeni kwa chama chake cha RPF.

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Kagame amepata asilimia 99.15 katika uchaguzi wa Rwanda.Picha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Katika uchanguzi wa bunge, chama hicho tawala na washirika wake wamefanikiwa kupata viti 37 kati ya viti 53,ikiwa ni kiwango cha chini kutoka wabunge 40 katika bunge la zamani.

Kagame apata ushindi wa kishindo uchaguzi wa Rwanda

Chama cha Habineza kiliweza kudhibiti nafasu yake ya viti viwili, huku vilivyosalia vikidhibitiwa na RPF na washirika wake. Katika taarifa yake ya Jumatatu jioni Tume ya Uchaguzi Rais Kagame alipata asilimia 99.18 ya kura zote zilizopigwa, na hivyo kumpa miaka mingine mitano madarakani.


 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW