1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaddafi Frankreich

Sekione Kitojo22 Februari 2011

Kiongozi wa mapinduzi nchini Libya muammar al-Gaddafi anakabiliwa na uwezekano wa kuangukia katika hatma kama iliyowakumba Ben Ali wa Tunisia na Hosni Mubarak wa Misr, kutokana na ukandamizaji

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alipojitokeza kusema kuwa hajaikimbia nchiPicha: AP

Kiongozi wa mapinduzi nchini Libya Muammar al-Gaddafi anakabiliwa na uwezekano wa kuangukia katika hatma kama iliyomkumba Ben Ali nchini Tunisia na Hosni Mubarak wa Misri , kabla ya kupigwa kumbo na hasira za umma kutokana na miongo kadha ya ukandamizaji, uingiliaji kati wa serikali ,pamoja na kukwama kwa maendeleo. Kama ilivyokuwa kwa tawala nyingine za kimabavu katika eneo hilo, Gaddafi pia alikuwa kwa muda mrefu mshirika muhimu wa baadhi ya serikali za mataifa ya magharibi katika masuala ya kiuchumi, licha ya kujihusisha kwa kiongozi huyo hapo zamani na matukio kadha ya kigaidi. Na ushirika huo ulikuwapo hata wakati Ufaransa ikiwa chini ya rais Chirac na Sarkozy.

Yaliwekwa mahema katika nje ya eneo la hoteli maarfu ya Marigny, iliyoko karibu kabisa na eneo la ikulu ya rais ya Elysee, ambayo ni makaazi ya rais. Muammar al Gaddafi alijisikia vizuri sana karibu na rafiki yake Nicolas Sarkozy, ambapo ziara iliyopagwa kuwa siku tatu ilifikia siku sita, wakati wa ziara yake Desemba 2007. Rama Yade, ambaye wakati huo alikuwa waziri anayehusika na haki za binadamu , alishangazwa na kuchukizwa na tukio hilo. Ufaransa haipaswi kulamba miguu, iwe kwa kiongozi, ama kwa gaidi ama la , na kufuta damu katika miguu ya mhalifu.

"Natimiza tu wajibu wangu, hilo ndio jukumu langu. Ni kitu gani watu walisema ,wakati nikiwa waziri anayehusika na haki za binadamu"?

Aliyekuwa waziri anayehusika na haki za binadamu nchini Ufaransa Rama YadePicha: picture-alliance/dpa

Rama Yade alifanyakazi wakati huo kama kibao cha kuzolea taka kilichotumiwa na utawala. Alitaka kutoa ufafanuzi kutokana na maoni ya Wafaransa kiasi cha asilimia 61, pamoja na wapinzani ambao walishangazwa. Sarkozy anafanya ushirika wa kibiashara na mhalifu kutoka Tripoli. Mwishoni mwa mapumziko hayo katika mahema , makampuni ya Ufaransa yalifunga mikataba ya karibu euro bilioni kumi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kinu cha kinuklia kwa ajili ya Libya, mtambo wa kuchuja maji ya chunvi na kuwa ya kawaida, na ndege 21 za kiraia za Airbus. Kazi iliyobaki Sarkozy alimwachia mshirika wake mkubwa katika serikali , waziri mkuu Francois Fillon.

"Ufaransa imemwalika kanali Gaddafi, kwa kuwa kanali Gaddafi aliwaacha huru wauguzi kutoka Bulgaria. Na kwa kuwa kanali Gaddafi ameirejesha nchi yake katika jumuiya ya kimataifa. Wale wanaotaka sana kutupatia msaada wa mafunzo, wanapaswa kutoa kauli za tahadhari."

Aliyekuwa waziri mkuu wa Ufaransa Francois FillonPicha: AP

Nusu mwaka uliopita wauguzi watano kutoka Bulgaria walihukumiwa kifo nchini Libya , pamoja na daktari wa Kipalestina. Walituhumiwa kwa kuhusika na kuwaambukiza watoto 400 na virusi vya ukimwi. Nicolas Sarkozy ambaye amechaguliwa wakati huo kuwa rais wa Ufaransa aliiona nafasi hiyo, na kulazimisha kuanzisha umoja wa nchi zinazopakana na bahari ya Mediterranean. Alimtuma wakati huo aliyekuwa mkewe Cecilia mjini Tripoli. Madame Sarkozy alilakiwa na Gaddafi, na siku chache wauguzi hao wakaachiwa huru.

"Cecilia amefanya kazi nzuri sana.Kulikuwa na tatizo na sasa tumelitatua. Hatukulitatua sisi wenyewe tu, lakini tumelitatua kwa pamoja. Na hili ndio suala ambalo ni muhimu."

Siku moja baada ya kuachiliwa wauguzi hao , Sarkozy na Gadaffi walifikia makubaliano juu ya mikataba ya mabilioni ya euro mjini Tripoli, mikataba ambayo ilitiwa saini miezi sita baadaye mjini Paris. Msingi mkubwa wa ukaribiano huu uliwekwa na mtangulizi wa Sarkozy , Jacques Chirac. Kabla ya umoja wa mataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Libya mwaka 2003, Chirac alikwenda Tripoli. Lakini mwaka 2005 kiongozi wa kwanza kuzuru Libya alikuwa waziri wa zamani wa ulinzi Michelle Alliot-Marie, ambaye hii leo anashutumiwa kutokana na uhusiano wake mzuri na utawala ulioangushwa nchini Tunisia wa Ben Ali.

Mwandishi : Wöss, Christoph / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Thelma Mwadzaya

.