1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usimamizi wa maji Ujerumani: Kati ya mafuriko na ukame

20 Julai 2021

Kwa muda sasa kumekuwa na uvumi kuhusu ukame nchini Ujerumani, na sasa mikoa mingi imefunikwa na maji. Ni kwa namna gani mamlaka zinajiandaa kwa ajili ya matukio hayo mawili? Mafuriko ya karibu yamemulika hali hii.

Deutschland Schäden nach Starkregen in Ahrweiler
Picha: Abdulhamid Hosbas/AA/picture alliance

Nchini Ujerumani, usimamizi wa maji na majitaka ni wajibu wa manispa za miji na majiji. Baadhi yake zimeunda hata vyama kuboresha ufanisi. Kwa mfano, manispa katika wilaya ya Euskirchen na maeno mengine hadi kwenye mpaka wa Ujerumani na Uholanzi zimeungana na kuunda chama cha maji cha Eifel-Rur (WVER).

Kimsingi Ujerumani ina maji zaidi ya kutosha kutoa majumbani na hata viwandani. Mamlaka zenahesabu wastani wa mita bilioni 188 za ujazo, ambazo ni sawa na madumu karibu trilioni 50 katika kipindi cha muda mrefu -- hii ni wingi wa mara mbili zaidi ya maji ya ziwa Geneva.

Mnamo mwaka 2016 kwa mujibu wa ofisi ya takwimu ya shirikisho, asilimia 13.5 ya kiwango hiki ilivunwa. Sehemu kubwa ya maji hayo yalitumiwa viwandani, kwenye kilimo au kupooza mitambo, na siyo kama sehemu ya ugavi wa maji kwa umma.

Soma pia: Merkel atembelea jimbo lingine lililokumbwa na mafuriko

Uvunaji wa kila mwaka wa hadi asilimia 20 unachukuliwa kutokuwa tatizo. Lakini tangu mwaka 2011, ugavi uliopo wa maji umebakia kuwa chini ya kiwango kilichokokotolewa - mwaka 2018, Ujerumani ilikuwa na karibu mita bilioni 119 za ujazo wa maji yaliopo kama rasilimali jadidifu.

Baada ya misimu mitatu mfululizo ya joto kali na ukame, baadhi ya wataalamu walionya mwezi Januari kwamba udongo nchini Ujerumani ulikuwa karibu umekauka kabisaa. Sasa, alau kwa muda, mamlaka za maji zinapambana kukabiliana na kinyume kilichopitiliza.

Ukuta wa nyuma wa bwawa la Steinbachtalsperre ukiwa umaharibiwa vibaya.Picha: Sebastien Bozon/Getty Images/AFP

Mabwawa ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanarikodi viwango cha chini vya maji yamefura kiasi cha kupasuka. Kwa siku kadhaa baada ya mafuriko, hali ya bwawa la Steinbach katika wilaya ya Euskirchen limesababisha wasiwasi.

Baadhi ya miji na vijiji vilivyopo chini ya bwawa hilo vilihamishwa, kwa sababu ilikuwa inachukuwa muda mrefu kupunguza maji yanayoelemea bwawa hilo. Wakaazi wanaweza kurejea makwa siku ya Jumatatu.

Wajibu wa kuzuwia mafuriko

Kwa muongo usiopungua moja sasa, kumekuwepi na agizo la Umoja wa Ulaya kuzitaka nchi wanachama kusimamia hatari za mafuriko. Nchini Ujerumani, usimamizi kimsingi uliachwa kwa majimbo mmoja mmoja.

Soma pia: Je mabadiliko ya tabia nchi yamechangia mafuriko?

Kwa mfano, jimbo la Rhineland-Palatinate, ambalo liliathiriwa vibaya hasa na mafuriko, huandaa tathmini za hatari na mipango na kujenga hatua za ulinzi kama vile mifereji kwenye njia kubwa za maji kama vile mito Rhine na Moselle.

Shirika la mazingira la Ujerumani UBA, hivi karibuni lilitathmini hatua zilizochukuliwa kote nchini juu ya mito muhimu zaidi kama zenye ufanisi. Na kwa kweli, viwango vya maji vya mto Rhine havikusababisha matatizo makubwa wakati wa janga la karifuni.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akitembelea moja ya maeneo yalioathiriwa vibaya na mafuriko katika jimbo la North Rhine-Wesphalia, akiwa pamoja na waziri mkuu wa jimbo hilo Armin Laschet, Julai 20, 2021.Picha: Wolfgang Rattay/AFP/Getty Images

Mito ambayo mafuriko yake yalisababisha uharibifu mbaya zaidi -- wa Ahr na Kyll katika jimbo la Rhineland-Palatinate na Erft jimboni North Rhine-Westphalia, ni njia ndogo  tu za maji. Na hapo manispaa ndiyo zinawajibika kutekeleza hatua za ulinzi dhidi ya mafuriko.

Kutokana na mzozo wa tabianchi, hali hizi mbili zilizopitiliza - yaani maji mengi sana au machache sana - zitajitokeza mara kwa mara nchini Ujerumani katika siku za usoni. 

Soma pia: Vifo kutokana na mafuriko Ulaya vyapindukia 150

Mzozo wa tabianchi walaazimu mageuzi

Ili kuianda nchi kwa changamoto hizo, waziri wa mazingira Svenja Schulze, ametangaza mkakati wa kitaifa wa maji. Mkakati huo unalenga kuyafanya maziwa na mito kuwa safi zaidi na yenye afya, kufanyia mageuzi usimamizi wa maji na kuzuwia uhaba wa maji. 

Moja ya dhana zake ni kuwa na bei janja za maji ambazo zinarahisisha matumizi ya maji wakati wa vipindi vya mahitaji madogo. Pia unapendekeza kuundwa mifumo itakayoamua nani atakuwa na kipaumbele cha kutumia maji, wakati eneo makhsusi linakabiliwa na upungufu.

Mpango huo unatazamia uwekezaji wa karibu euro bilioni moja kufikia mwaka 2030, lakini bado unahitaji kuidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji na serikali ijayo. Kwa sababu hii, chama cha upinzani cha Kijani kimeutaja mkakati huo kuwa usiokuwa na maana ikiwa hautatekelezwa mwishowe.

Soma pia: Ujerumani yatakiwa kujiandaa zaidi dhidi ya majanga

Neno mji wa Sponji limetumiwa pia katika mpango huo. Kwa maneno mengine, unataka miji huko mbeleni iwe na maeneo tosha ya kijani, ambako maji yanaweza kunyonywa kwa urasihisi na kutiririka chini ya ardhi. Hii itamaanisha kuwa maji yatokanayo na nvua hayataishia moja kwa moja baharini kupitia mito.

Mwandishi:David Ehl

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW