1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usitishaji mapigano mashariki mwa Kongo waafikiwa

31 Julai 2024

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda umefikia makubaliano ya kipindi cha usitishwaji mapigano mashariki mwa Kongo kuanzia mwezi unaokuja.

Wanajeshi wa Kongo
Vikosi vya jeshi la Kongo vinapambana na waasi wa M-23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Picha: Al-hadji Kudra Maliro/AP Photo/picture alliance

Hayo yametangazwa na ofisi ya rais wa Angola, nchi hayo ambayo imekuwa mpatanishi katika duru kadhaa za mazungumzo ya kumaliza uhasama kati ya Kongo na Rwanda kuhusiana na vita vinavyoendelea mashariki mwa Kongo.

Serikali ya Kongo imekuwa ikiituhumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaoendesha hujuma mashariki mwa Kongo.

Kulingana na ofisi ya rais Joao Lourenco wa Angola, usitishaji mapigano utaanza usiku wa manane wa Agosti 4 na utaratibu utawekwa kusimamia utekelezaji wake.

Makubaliano hayo yamepatikana wakati wa mkutano wa mawaziri wa kigeni wa mataifa hayo mawili ulofanyika katika mji mkuu wa Angola, Luanda. Yameafikiwa wakati makubaliano mengine ya kusitisha mapigano chini ya misingi ya kiutu yanaelekea kufikia mwisho mnamo Agosti 3.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW