1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usitishaji wa mapigano kati ya Israel na Hezbollah waanza

27 Novemba 2024

Usitishaji vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Lebanon Hezbollah umeanza kutekelezwa leo.

Libanon Waffenruhe | Flüchtlinge Rückkehr in Süden
raia wameketi nyuma ya lori na mali zao wanapowasili katika mji wa Nabatieh, kusini mwa Lebanon, Novemba 27, 2024,Picha: MAHMOUD ZAYYAT/AFP

Wakaazi wameonekana wakisafiri kwenye magari yaliyojaa mali zao kurudi kusini mwa Lebanon licha ya onyo kutoka kwa wanajeshi wa Israel na Lebanon kwamba wasikae kwenye maeneo fulani. Kama utaheshimiwa kikamilifu, utafikisha mwisho karibu miezi 14 ya mapigano kati ya Israel na Hezbollah. Mpango huo uliosimamiwa na Marekani na Ufaransa, na kuidhinishwa jana jioni na Israel. Emmanuel Macron ni Rais wa Ufaransa. Makubaliano hayo yanatoa wito wa kusitishwa mapigano kwa miezi miwili kwanza na unawahitaji Hezbollah kusitisha uwepo wao kusini mwa Lebanon, wakati askari wa Israel wakirejea kwenye upande wao wa mpaka. Maelfu ya askari wa ziada wa Lebanon na walinda amani wa Umoja wa Mataifa watapelekwa kusini, na jopo la kimataifa linaloongozwa na Marekani litafuatilia utekelezaji huo. Viongozi mbalimbali wa dunia wamepongeza makubaliano hayo wakitoa wito wa kutekelezwa kikamilifu. Naye afisa wa Hamas Sami Abu Zuhri ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kufuatia makubaliano hayo ya Israel na Hezbollah, Hamas pia wako tayari kusitisha vita na Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW