1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benki ya Credit Suisse kuomba mkopo wa dola bilioni 54

16 Machi 2023

Benki ya kimataifa ya vitega uchumi ya Uswisi, Credit Suisse, imesema itaomba mkopo wa dola bilioni 54 kutoka benki kuu ya nchi hiyo kwa lengo la kuimarisha ukwasi wa benki hiyo na kuhakikisha usalama wa amana za wateja.

Finanzmarkt Credit Suisse Logo
Picha: Fabrice Coffrini/AFP

Benki hiyo pia itachukua deni la dola bilioni 2.5 na vilevile italipa deni la Euro milioni 500 ili kurejesha faida kwa wawekezaji. Hisa za benki hiyo zilianguka kwa aslimia 24 hapo jana baada ya kugundulika udhaifu katika taarifa zake za fedha.

Matatizo ya benki hiyo yalijitokeza wiki iliyopita baada ya benki kubwa ya Marekani ya Silicon Valley kusambaratika, pamoja na uamuzi wa mwekezaji mkuu ambaye ni benki ya Saudi Arabia kukataa kuongeza fedha zaidi kwa ajili ya benki hiyo ya Uswisi.

Misukosuko ya benki hiyo imesababisha wasiwasi juu ya mfumo wa fedha barani Ulaya kama mgogoro mkubwa wa mabenki uliotokea mnamo mwaka 2008.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW