1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti: Borussia Dortmund ni klabu maarufu zaidi Ujerumani

15 Desemba 2022

Borussia Dortmund ndio klabu maarufu zaidi ya kandanda nchini Ujerumani baada ya kuipiku Bayern Munich, kulingana na utafiti uliochapishwa Jumatano.

Fussball I Bundesliga I Borussia Dortmund - VfL Bochum
Picha: Ina Fassbender/AFP

Usimamizi wa kampuni ya SLC mjini Nuremberg umesema klabu ya Dortmund inaongoza kwa umaarufu, ikifuatiwa na mabingwa wa ligi kuu ya Bundesliga Bayern Munich, kwa mara ya kwanza tangu waazishe utafiti huo miaka minane iliyopita.

Utafiti huo ulizingatia vigezo 18, kama vile idadi ya wanachama wa klabu, wingi wa mashabiki, watazamaji wa runinga na wafuasi wa mitandao ya kijamii na kuhusisha Wajerumani 30,000.

Washindi wa ligi ya Ulaya Eintracht Frankfurt ni ya tatu katika umaarufu, mbele ya Borussia Mönchengladbach. Hertha Berlin imeshuka kutoka nafasi ya nane hadi 15 huku Bayer Leverkusen ilipanda kutoka nafasi 17 hadi 11.

Greuther Fürth iliyoshushwa daraja ni ya mwisho, nyuma ya Augsburg.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW