1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti: Hotuba hasi za kisiasa zaongezeka Marekani

Hawa Bihoga
24 Novemba 2023

Utafiti ulioongozwa na Maabara ya Sayansi ya Takwimu Uswisi, unaonesha tangu Trump alipozindua kampeni zake za urais kwa mara ya kwanza matamshi hasi ya kisiasa yaliongezeka Marekani.

USA Donald Trump Rede beim CWALAC-Gipfel in Washington
Picha: Leah Millis/REUTERS

Kura za maoni zinaonyesha Wamarekani wengi wanaamini mijadala ya kisiasa imezorota tangu rais wa zamani Donald Trump aingie kwenye jukwaa la kisiasa.

Katika wakati huu ambapo Trump anaendelea na mbio zake za kisiasa , watafiti wanasema taarifa zinathibitisha wapo sahihi.

Wakitumia kompyuta katika kuchambua  takriban nukuu laki tano za wanasiasa kutoka katika makala kwenye vyombo vya habari zilizochapishwa kwa zaidi ya muongo mmoja, watafiti kutoka Uswisi wanasema waligundua mwelekeo huo wa wazi..

Mnamo mwezi Juni 2015, mwezi ambao Trump alizindua kampeni zake za kuwania urais kwa mara ya kwanza, taarifa zinaonesha kuibuka kwa kiwango kikubwa cha "matamshi hasi"

Mtafiti Mkuu wa utafiti huo Robert West aliiambia shirika la habari la AFP.

Soma pia:Biden: Kampeni ya "Fanya Marekani Kuwa Kuu Tena" ni tishio kwa demokrasia

Trump alianzisha kampeni yake kwa kuwashambulia Waislamu, kumdhihaki ripota mlemavu na kuwaita wafanyakazi wa vyombo vya habari kuwa ni maadui wa watu, akitoa kauli zilizotafsiriwa za kuwadharau wanawake na kueleza kuwa unyanyasaji wa kisiasa unakubalika.

Tangu wakati huo maneno hayo yanaonekana kukubalika na ya kawaida katika ulingo wa siasa za Marekani.

West ambae ni profesa msaidizi akiongoza kitengo cha Maabara ya Sayansi ya Takwimu katika Taasisi ya Shirikisho ya Teknolojia ya Uswisi, alisema yeye na timu yake walishangazwa na matokeo ya kuraza maoni zilizoonesha kwamba, Wamarekani wengi wanaamini mijadala ya kisasa imekuwa si ya heshima na hasi zaidi.

Kanzidata ya matamshi hasi ya kisiasa

Utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Pew ulionyesha kuwa zaidi ya nusu ya waliohojiwa wanaamini, lawama zinapaswa kuelekezwa kwa Trump ambaye alihudumu kama raiskutoka 2016 hadi 2020 na anatarajia kushinda muhula mpya katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Wafuasi wa Trump waandamana Biden akiongoza uchaguzi

01:01

This browser does not support the video element.

"Tulidhani jambo kama hilo" alisema West na kuongeza kwamba "sisi ni watu wa takwimu, tulijuiliza tunaweza kuangalia takwimu zinasema kitu sawa na hicho?"

Walipoanza kuchunguza suala hilo muda mfupi baada ya Trump kushinda urais, waligundua kuwa hawakuwa na takwimu zilizobaini kisayansi jinsi matamshi makali ya kisiasa yalivyoibuka kwa wakati huo.

Soma pia:Chama cha Republican kimebakiwa na muda mfupi kabla ya kuanza mchakato wa kuteua mgombea wa urais

Hivyo waliamua kuanzisha kanzidata kubwa iliotambulika kwa Quotebank, ikihifadhi jumla ya nukuu milioni 235, zilizotolewa kwenye nakala za mtandaoni zipatazo  milioni 127, zilizochapishwa katika kipindi cha mwaka 2008 na 2020.

Ikiruhusu watafiti kufanya uchambuzi wa kina juu ya lugha na sauti  za wanasiasa wa Marekani kwa umma.

Matamshi hasi ya kisiasa yaongezeka kwa kasi

West alisema katika kipindi cha utawala wa aliekuwa rais wa Marekani Barack Obama kuanzia 2009 hadi 2016 ,mara zote maneno na hotuba kali katika ulingo wa kisiasa nchini humo zilipungua.

Rais wa zamani wa Marekani Donald TrumpPicha: Mike Mulholland/AP/picture alliance

Lakini mnamo mwezi June, wakati mwanasiasa na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipozindua kampeni zake hotuba kali za kisiasa ziliibuka kwa kasi na kufikia asilimia themanini ikilinganishwa na kiwango cha msingi katika miaka saba iliyopita.

"Kwakweli hilo ni ongezeko kubwa" West alisema .

"Na yalianza mwezi ambao Trumpa alizundua kampeni, kwa hiyo hii inaonesha alikuwa chanzo kwamba Trump alikuwa chanzo kwenye hili." Alisisitiza

"Unapoondoa nukuu za Trump, kiwango kinapungua na kushuka hadi asilimia arobaini." Aliongeza

Soma pia:Trump aususia mdahalo wa wanasiasa wa Republican

West alisema takwimu zilionyesha kuwa kunaweza kuwa na ongezeko lingine la matamshi hasi katikati ya 2019, wakati kampeni za Trump dhidi ya Rais wa sasa Joe Biden yaliongezeka.

Lakini bado haijulikani ikiwa hili ni ongezeko la muda wa kampeni, kwani ufikiaji wa timu kwenye takwimu mpya ulisimamishwa mnamo 2020.

Timu hiyo inatafuta ushirikiano mpya, na taasisi zingine kama Google au mashirika ya habari, ili kuweza kuongeza takwimu mpya na nukuu kwenye Quotebank yake.

Lakini hata bila takwimu mpya, West alisema matokeo hayo yalisaidia kuangazia jambo ambalo linaweza kuashiria demokrasia ya Marekani inadhoofika.

"Unahitaji kujua dalili ili kuponya ugonjwa," alisema.

Polisi Kenya kuwashitaki wanasiasa wachochezi

01:40

This browser does not support the video element.