Utafiti: kupungua kwa misaada kutasababisha vifo milioni 22
18 Novemba 2025
Matangazo
Zaidi ya watu milioni 22, wengi wao wakiwa watoto, wanaweza kufa kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika ifikapo mwaka 2030 kwa sababu ya kupunguzwa kwa misaadana Marekani na nchi za Ulaya, kwa mujibu wa utafiti mpya. Matokeo haya ni nyongeza ya utafiti wa awali ulioangazia misaada ya Marekani pekee na kusema kuwa kupunguzwa kwa kiwango kikubwa na Rais Donald Trump kungeweza kusababisha vifo vya ziada vya watu milioni 14.